Terms and Conditions

Kuhusu Kimondo Financial Services Limited

Kimondo Financial Services Limited ni Kampuni iliyosajiliwa na Brela (Na. ya Usajili 137-283-263) na kuanzishwa tangu mwaka 2018 chini ya sheria ya usajili wa makampuni ya Tanzania. Kimondo Financial Services Limited ni miongoni mwa taasisi za kifedha zilizopewa leseni nchini Tanzania inayotoa huduma mbalimbali za mikopo kwa watu binafsi na biashara ndogo ndogo. Kampuni inalenga kuridhisha wateja wake kwa kutoa huduma bora za kiwango cha juu. Bidhaa na huduma zote zinatolewa kwa bei shindani na huduma kwa wateja inahifadhiwa kwa kiwango cha juu. Kampuni inasimamiwa na Bodi ya Wakurugenzi yenye weledi na ina mameneja na wafanyakazi waliobobea wanaofanya kazi kwa ushirikiano ili kuiendeleza taasisi.

1.1 DIRA

Kuwa mtoa huduma za kifedha anayechaguliwa zaidi nchini Tanzania.

1.2 DHIMA

Kutoa suluhisho la mikopo midogo ili kubadili maisha ya watu kwa kutoa huduma bora za kifedha.

1.3 MALENGO

  1. Kutoa fursa ya upatikanaji wa huduma za kifedha kwa watu ili kuboresha maisha yao.
  2. Kutoa nafasi kwa watu kuongeza uwezo wao wa kifedha na kujenga uwezo wa kujitegemea kifedha.
  3. Kutoa huduma za kifedha kwa watu ambao hawana au wana upatikanaji mdogo kwa taasisi rasmi za kifedha kama benki kutokana na kipato chao kuwa kidogo, kisichoeleweka au kisicho cha kudumu.
  4. Kutoa mikopo ya haraka ili kukidhi mahitaji ya dharura ya watu.

1.4 MAADILI YA MSINGI

1.4.1 Bidii

Kampuni inatambua na kuthamini juhudi za watu binafsi na timu kwa msingi wa utendaji wa kuthibitishwa. Uaminifu na matokeo ni funguo za mafanikio ya kampuni.

1.4.2 Ubunifu

Kampuni inaamini katika kuanzisha mawazo mapya, mbinu mpya na taratibu mpya ili kuboresha utoaji wa bidhaa na huduma zake.

1.4.3 Uwajibikaji wa Kijamii

Kimondo inafanya kazi kwa maadili na kuchangia katika kuboresha maisha ya watu, jamii na taifa kwa ujumla.

1.4.4 Umakini kwa Wateja

Lengo letu kuu ni kuzidi matarajio ya wateja wetu katika utoaji wa huduma ili kupata imani na uaminifu wao. Kwa sababu hiyo, tunajali, tunaheshimu na tunajibu kwa weledi na maadili ya kijamii.

1.4.5 Kuaminika

Uadilifu na kutegemewa, tunazingatia ukweli na kuwa waaminifu kwa misingi imara ya maadili, tukiwa tumejidhatiti katika kuheshimiana tunapohudumia wateja wetu.

Sera ya Faragha

Tunakusanya aina zifuatazo za taarifa zako binafsi:

Jinsi Tunavyokusanya Taarifa

Tunakusanya taarifa zako kupitia:

Matumizi ya Taarifa Zako

Tunakusanya na kutumia taarifa zako kwa madhumuni yafuatayo:

Kushiriki Taarifa

Tunaweza kushiriki taarifa zako kwa:

Usalama wa Taarifa Zako

Tunatumia hatua za kiusalama kulinda taarifa zako dhidi ya upotevu, wizi, au ufikiaji usioidhinishwa.

Muda wa Kuhifadhi Taarifa

Tunahifadhi taarifa zako kwa muda unaohitajika kutoa huduma zetu na kufuata sheria. Baada ya muda huo, taarifa zitafutwa kwa njia salama.

Haki Zako

Una haki zifuatazo kuhusu taarifa zako binafsi:

Mabadiliko ya Sera ya Faragha

Tunaweza kufanya mabadiliko kwenye sera hii wakati wowote. Tutaweka taarifa ya mabadiliko haya kwenye tovuti yetu au kukutumia taarifa moja kwa moja.

Mawasiliano

Kwa maswali yoyote kuhusu sera hii ya faragha, tafadhali wasiliana nasi kupitia:

Jinsi ya Kurejesha Mkopo

Kakitu Loan

Mkopo huu unapatikana ndani ya dakika kumi (10) Kuanzia Tzs.20,000.00 mpaka kiasi cha Tzs.1,000,000.00. Riba ya mkopo huu ni asilimia 3.5%. Gharama ya mkopo huu ni asilimia 15% kwa wiki. Muda wa mkopo huu ni wiki moja tu.

Mkopo wa Binafsi/Biashara

Unatolewa kwa watu wote mfanyabiashara na mfanyakazi. Mkopo huu unatolewa ndani ya muda usiozidi siku tatu. Mkopo huu unaweza kuupata wakati wowote katika juma (Jumatatu-Jumamosi). Riba ya mkopo huu ni asilimia 3.5% kwa mwezi. Gharama ya mkopo huu ni asilimia 7% kwa mwezi na italipwa mara moja tu. Muda wa mkopo huu ni miezi sita.

Vigezo na Masharti

Kuhusu Mkopo wa Kawaida (Binafsi)

Unatolewa kwa watu wote mfanyabiashara na mfanyakazi. Mkopo huu unatolewa ndani ya muda usiozidi siku tatu. Mkopo huu unaweza kuupata wakati wowote katika juma (Jumatatu-Jumamosi). Riba ya mkopo huu ni asilimia 3.5% kwa mwezi. Gharama za mkopo huu ni asilimia 7% kwa mwezi na italipwa mara moja tu. Muda wa mkopo huu ni miezi sita.

Kakitu Loan

Mkopo huu unapatikana ndani ya dakika kumi (10) Kuanzia Tzs.20,000.00 mpaka kiasi cha Tzs.1,000,000.00. Gharama ya mkopo huu ni asilimia 10% kwa wiki. Muda wa mkopo huu ni wiki moja tu.

Mkopo wa Bima

Ni mkopo unaotolewa kwa ajili ya kumkatia mteja bima katika kampuni za bima bila kuweka dhamana. Mteja atachangia asilimia 30% ya gharama ya bima kabla ya kukatiwa bima. Gharama za mkopo ni asilimia 7%. Muda wa mkopo huu ni miezi minne tu.

Bima Ndogo

Bima hii ni bima ya lazima kwa wamiliki wote wa magari, huhusiana na ajali za barabarani zinazosababishwa aidha na mmiliki wa gari au dereva wa gari husika. Bima hii inatoa wajibu wa kumfidia aliyeumia kwenye ajali. Muathirika wa ajali anaweza kudai fidia.

Bima Kubwa

Hi ni aina ya bima inayolinda gari yako pindi ikipata ajali, wizi, au kuungua moto taasisi ya bima itamlipa fidia dhidi ya muathirika na muathiriwa wa ajali.

Company Profile

KIMONDO FINANCIAL SERVICES LIMITED ni kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria ya usajili wa makampuni ya Tanzania mwaka 2018. Kampuni hii inajihusisha na utoaji wa mikopo kwa wafanyakazi, waajiriwa, Kampuni na mtu mmoja mmoja.

Sifa za Mtumiaji (Terms & Conditions)

Mchakato wa Maombi ya Mkopo

Viwango vya Riba na Ada

Malipo ya Mkopo

Usalama wa Taarifa

Matumizi ya Programu

Mabadiliko ya Masharti

Sheria na Migogoro

Kwa kutumia programu hii, unathibitisha kuwa umesoma na kuelewa masharti haya na unakubali kuyafuata. Nakubali kwamba, Mkopeshaji anaweza kutafuta taarifa zangu zinazohusiana na mikopo kutoka Taasisi ya taarifa za mikopo (Credit Reference Bureau) muda wowote bila kulazimika kutafuta ridhaa yangu. Vilevile, mkopeshaji anaweza kupeleka taarifa zangu za mkopo katika taasisi ya inayohusika na taarifa za mikopo (Credit Reference Bureau).

Jinsi ya Kufanya Malipo

Unaweza kufanya malipo yako ya marejesho kupitia Tigo Pesa, M-Pesa, Airtel Money na CRDB Bank ACCOUNT NO: 0150396688000 Kimondo Financial Services.

Jinsi ya Kufanya Malipo Tigo Pesa

  1. Piga *150*01#
  2. Chagua chaguo 4 lipia bili
  3. Chagua chaguo 3 Ingiza Namba ya Kampuni
  4. Ingiza namba ya Kampuni 889999
  5. Weka kumbukumbu ya malipo (Namba yako ya Mkopo)
  6. Ingiza kiasi
  7. Ingiza Namba ya siri

Jinsi ya Kufanya Malipo Airtel Money

  1. Piga *150*60#
  2. Chagua chaguo 5 lipia bili
  3. Chagua chaguo 2 chagua Kampuni
  4. Chagua chaguo namba 7 Chagua kampuni
  5. Weka Namba 47
  6. Ingiza namba ya kumbukumbu (Namba yako ya mkopo)
  7. Weka kiasi
  8. Ingiza 1 (Ndio) kuthibitisha
  9. Weka PIN

Jinsi ya Kufanya Malipo M-Pesa

  1. Piga *150*00#
  2. Chagua chaguo 4 lipi kwa Mpesa
  3. Chagua chaguo 4 weka namba ya Kampuni
  4. Ingiza namba ya Kampuni 310745
  5. Weka kumbukumbu ya malipo (Namba yako ya mkopo)
  6. Ingiza kiasi
  7. Weka namba yako ya Siri
  8. Weka 1 kuthibitisha