1. Utangulizi
Kimondo Financial Services Limited inakukaribisha kutumia Kimondo App inayokuwezesha kukopa fedha moja kwa moja na kwa urahisi. Kampuni imesajiliwa na BRELA (Na. ya Usajili 137-283-263) na kuanzishwa mwaka 2018 chini ya sheria ya makampuni ya Tanzania.
Kimondo Financial Services Limited ni taasisi ya kifedha yenye leseni inayotoa huduma za mikopo kwa watu binafsi na biashara ndogo ndogo. Kampuni inalenga kutoa huduma bora, nafuu, na salama kwa wateja wake, ikisimamiwa na bodi yenye weledi na timu ya wataalam.
Ili kuongeza ufanisi na urahisi wa kutoa huduma kwa wateja wetu, Kimondo Finance inapenda kukukaribisha kutumia Kimondo App, Application ambayo itakuletea huduma zetu kiganjani mwako. Kwa kuendelea kutumia Application ya Kimondo, utakuwa umekubaliana na makubaliano haya ya huduma. Kama haujakubaliana nayo tafadhali usiendelee.
2. Wajibu Wako Mkopaji
- Kuwa na umri usiopungua miaka 18 na mwenye akili timamu.
- Kuwa na Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
- Kujisajili kwa kutumia taarifa sahihi.
- Kulinda akaunti yako na OTP dhidi ya matumizi mabaya.
- Kukubaliana na masharti ya huduma haya kwa hiari.
3. Huduma / Aina za Mikopo
Mikopo Binafsi: kwa wafanyabiashara na wafanyakazi, muda wa miezi 6, riba 3.5% kwa mwezi, ada 7%, adhabu ya kuchelewa 1.5% kwa siku.
Mikopo ya Bima: mteja huchangia 30% ya gharama ya bima, muda wa miezi 4, riba 3.5% kwa mwezi, ada 7%, adhabu ya kuchelewa 1.5% kwa siku.
Kakitu Loan: mkopo wa haraka ndani ya dakika 10, hadi Tsh 1,000,000, riba 0.88% kwa wiki, ada 15% kwa wiki, muda wiki moja, adhabu ya kuchelewa 1.5% kwa siku.
4. Namna ya Kufanya Marejesho
Malipo yanaweza kufanywa kupitia benki au mitandao ya simu.
5. Haki ya Mkopeshaji
- Kubadilisha au kukataa maombi ya mkopo bila maelezo.
- Kuomba taarifa za ziada za kuthibitisha maombi.
6. Taarifa Binafsi
Kimondo App hukusanya taarifa za mtumiaji (jina, nambari ya simu, anwani) kwa ajili ya huduma, mawasiliano, na ufuataji wa matakwa ya kisheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
7. Haki Miliki
Nembo, maudhui, picha, na mfumo wa App ni mali ya Kimondo Financial Services Ltd. Matumizi ya kibiashara bila idhini ni marufuku.
8. Ulinzi
Ni marufuku kutumia App kwa njia zisizo halali kama kudanganya taarifa, kuwa na akaunti nyingi, au kuvunja sheria za Tanzania. Ukiukaji unaweza kusababisha kufutwa kwa akaunti na hatua za kisheria.
9. Haki za Mtumiaji
- Kuomba mkopo na kusitisha mkopo.
- Kuomba kufutwa kwa taarifa binafsi kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
- Kuchagua njia ya malipo na kupokea taarifa za mabadiliko ya huduma.
10. Ada Zinazochajiwa
Ada za huduma zinaweza kutozwa na mtumiaji ataarifiwa mapema kabla ya kutozwa.
11. Mabadiliko ya Vigezo
Kimondo App ina haki ya kufanya mabadiliko kwenye makubaliano haya na mtumiaji ataarifiwa kupitia ujumbe mfupi au App.
12. Mawasiliano
Kwa mawasiliano: Simu/WhatsApp: +255677090901 / +255677090902
Instagram/X/TikTok/Facebook: @Kimondofinance
Barua pepe: info@kimondofinance.co.tz
Tovuti: www.kimondofinance.co.tz